Picha: Chaby Six afunga ndoa kimya kimya

0

Msanii wa muziki wa hip hop kutokea Mboriborini, Chaby Six amefunga ndoa kimya kimya na mpenzi wake wa muda mrefu ijumaa iliyopita (Jan 27).

Rapa huyo ambaye kwa sasa yupo kimya kwa muda mrefu bila ya kuachia wimbo mpya amekuwa ni msanii wa pili ndani ya mwezi huu kufunga ndoa baada ya Januari msanii Kinde Makengele kuvuta jiko.

Baadhi ya wasanii pamoja na wadau mbalimbali wa muziki wamepongeza msanii huyo kwa hatua aliyofikia.