Picha: Blue, Barnaba na Linex walivyopagawisha Zanzibar

0

Usiku wa kuamkia Jumamosi Disemba 3,Wasanii kutoka Dar es Salaam Mr. Blue, Barnaba na Linex walifanya onyesho la kufungia mwaka katika ukumbi wa CCM Maisara.

Katika onyesho hilo msanii Jumaa Town alifungua show hiyo akiwa na ‘madancer’ wake ambapo mzuka uliwapanda madancer hao na kuvunja steji ambalo walilokuwa wakilitumia kwa ajili ya onyesho lao.

Baada ya hapo ilifuatiwa na Live Band kutoka kwa Barnaba na Linex na mwisho Mr Blue alimalizia onyesho hilo.