P. Diddy atangaza kustaafu muziki rasmi atakapoachia albamu ya ‘No Way Out 2’

0

Ikiwa ni kama kauli mbiu yake P.Diddy “Siwezi kusimama na sitosimama” lakini inaonekana ni tofauti kabisa kwa boss huyo wa Bad Boy ambapo alitoa taarifa ya kustaafu muziki.

Akiwa katika mahojiano, Puff Daddy alielezea kwanini albamu yake ijayo ya No Way Out 2, itakuwa ndio albam yake ya mwisho katika muziki wa rap.

“Nataka kuachia albamu yangu ya mwisho na kujishughulisha kwa asilimia mia moja ya muda wangu kwenye filamu” alisema Diddy. Pia aliongezea ” Nataka nistaafu nikiwa katika nafasi nzuri… Albamu yangu ya mwisho ndio sehemu nzuri ya kustaafu, nataka nimalize nikiwa ┬ákama mshindi, na nifurahie kufanya show zangu za kuzunguka dunia kwa mara ya mwisho kwenye muziki.”

Diddy ameahidi kuwa NWO2 itakuwa nzuri na itakuwa ina sehemu muhimu za kumbukumbu yake ya kuwa katika muziki kwa miaka 20.

“Nitakapoondoka, nyimbo zangu bado zitaendelea kuwepo, najua natengeneza muziki ambao utaishi kwa muda mrefu. Siendi studio kwa kutaka kujisikiliza mwenyewe kwenye redio. Michael Jackson, Tupac, Biggie miziki yao bado ipo, japokuwa wao hawapo kabisa na yote inayofanya hivyo ni imani.”

Hii si mara ya kwanza kwa P.Diddy kutangaza kustaafu muziki. Alishawahi sema kama hiyvo mnamo mwaka 2004 ” nimeshaipata nafasi ambayo ya ndoto yangu kuwa kweli, nataka kuhakikisha kuwa nafanya maamuzi nitakapoachia albamu yangu ya mwisho.”