Mkongwe wa muziki wa Pop ‘Prince’ Afariki dunia

0
prince

Prince Rogers Nelson, anajulikana kama mwanamuziki mkongwe anayetumia jina la ‘Prince’ ameiaga dunia leo Alhamis akiwa na umri wa miaka 57 na bila kujulikana chanzo cha kifo chake.

Kupitia mtandao wa TMZ, mkongwe huyo ameonekana ameshafariki akiwa nyumbani kwake Paisley Park mjini Minnesota, Marekani. Na kifo hicho kilithibitishwa na chombo cha habari kuhusiana na kifo hicho kilichotokea asubuhi ya leo.

Hali yake kiafya ilianza kuripotiwa kutokuwa sawa mnamo April 15, baada yake ndege binafsi kutua kwa dharura huko mjini Illinois na kumuwahisha katika kituo cha matibabu ambapo kilieleza kuwa nyota huyo alikuwa akisumbuliwa na mafua makali. Lakini baadae alifanikiwa kufanya onyesho lake siku ya pili yake na kuwaondoa mashabiki kwa kusema yupo sawa kiafya.

Prince alianza kujizolea umaarufu mnamo mwaka 1978 alipokuwa na miaka 19 ambapo aliachia albamu yake ya kwanza ‘Putting out for you’. Angalia moja ya wimbo wake uliokuwemo katika albam hiyo.