Nick Cannon na mchumba wake wapata mtoto wa kiume

0

Hongera nyingi zinaenda kwa Nick Cannon na mchumba wake Britanny Bell ambapo mnamo Feb. 21, Brittany Bell amejifungua mtoto wa kiume na kumpa jina Golden ‘Sagon’ Cannon.

Mtangazaji huyo wa kipindi cha luninga cha “Wild ‘N Out” amesherehekea taarifa hiyo baada ya kuweka picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa amemshikilia mwanawe  na kuandika:

“Weeping may endure for a night, but Joy cometh in the morning, No matter how hard the world may hit you, God always reminds us of our purpose! #TrueHappiness Welcome to Earth Son!”

Golden Cannon atakuwa ni mtoto wa tatu kwa Nick Cannon ambapo tayari alishazaa na ex wake Mariah Carey watoto mapacha wawili wenye umri wa miaka mitano, Moroccan na Monroe.