(Ni Vijimambo tu): Rais Joseph Kabila Amfukuza Kazi Naibu Waziri wa Mawasiliano wa Congo Kwa Kosa la Kupiga Punyeto Ofisini

0
rais
Rais Jamhuri wa Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila amemtimua kazi Naibu Waziri wa Posta na Mawasiliano Mhe.Enock Ruberangabo kutokana na kusambaa kwa video inayomuonesha akipiga punyeto ofisini
Kwa mujibu wa televisheni ya taifa, RTNC, Kabila amedai waziri huyo, Enock Ruberangabo Sebineza ameliabisha taifa.
Tangu Alhamis iliyopita hadi Ijumaa, video hiyo imekuwa ikisambaa mtandaoni ikimuonesha waziri huyo akijichua ofisini kwake. Nyuma yake inaonekana bendera ya nchi hiyo na picha ya Rais Kabila.
Wananchi wengi wamekasirishwa na video hiyo na kumtaka ajiuzulu.