Categories
Music

New Music: Zanzibar Fleva Unit waachia wimbo mpya “Corona ni Hatari”

Umoja wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Zanzibar Flava Unit wameachia wimbo mpya ambao unaozungumzia dhidi ya ugonjwa hatari wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Akizungumza na Zenji255 Raisi wa ZFU Laki, amesema kuwa kutengeneza wimbo huo kwetu tumeona ni vizuri ili kuweza kuhamasisha jamii yetu ya Zanzibar na duniani kwa ujumla juu ya kujikinga na virusi vya Corona.

“Kiukweli virusi vya Corona vinasambaa kwa haraka sana, na kwa hapa tulipofikia sasa inabidi jamii ikae katika uangalizi mzuri. Kwanza, kujikinga. Pili, kuelemisha. Na ndio maana tukaamua kukaa chini na kutengeneza wimbo huu ambao ni burudani, lakini ndani yake kuna ujumbe wa kuhusu virusi hivyo” Raisi Laki.

Katika wimbo huo wameshiriki wasanii kama Nedy Music, Baby J, Chaby Six, Abramy, Zenji Boy, Sultan King, Rico Single, Sapna, Pozza Boy, Smile, Yoram na Laki wa Promise.

Sikiliza wimbo huo na utoe maoni yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.