Nassir Vanillah kuachia ‘Najuta Kuoa’ hivi karibuni

0

Msanii Nassir vanillah haijulikani yamemkumba nini kutokana na wimbo wake mpya ‘Najuta Kuoa’ anaotarajia kuuachia hivi karibuni.

nassir vanillahNassir miezi kadhaa iliyopita alifunga ndoa na mpenzi wake na kuamua kupumzika kufanya shuhuli za muziki kwa muda lakini katika ujio wake mpya umewafanya mashabiki kuwa na maswali mengi kichwani.

Akizungumza na Zenji255 Nassir amesema kuwa “Kwa sasa kikubwa nitakachozungumza ni kuhusiana na ujio wa wimbo wangu mpya wa Najuta Kuoa kwani tayari mipango yote ishamalizwa na tunasubiria siku tu ifike utasikia nini nilichozungumza katika huo wimbo.” Amesema “sitopenda kuulizwa maswali yanayohusiana na mahusiano ya ndoa yake kwani sipo tayari kulizungumzia hilo.”