Nassir Vanillah atarajia kuzindua wimbo na video mpya wikiendi hii

0

Msanii wa muziki Nassir Vanillah, kwa muda mrefu mashabiki walikuwa katika mkao wa kula wakisubiri ujio wa wimbo wake mpya ‘Najuta Kuoa’ ambao uliotakiwa kuachiwa mwaka jana mwishoni na matokeo yake kubadili mawazo na kuja na wimbo mwingine.

nassir

Akiongea na Zenji255 Nassir, ambaye siku ya Jumamosi (Feb. 25) anatarajia kuzindua wimbo na video yake mpya unaoitwa ‘Biringe Baikoko’ amesema wazo la wimbo wa Najuta kuoa bado lipo ila amefikiria kulisogeza mbele na atauachia baada ya wimbo huu wa sasa kuuachia.

“Kwa sasa najuta kuoa itasubiri kidogo” Amesema Nassir Vanillah “Biringe Baikoko ndio wimbo ambao utakaoruka hewani, na tayari video na wimbo wenyewe upo ambapo tarehe 25 tunauzindua Intebe. Wimbo na video umesimamiwa katika studio¬† za Tiffu Records na D. Sam ndie aliyehusika katika matayarisho ya video na wimbo wenyewe” Amesema Nassir Vanillah.