Nassir Vanillah asema ndoa sio sababu ya msanii kushuka kimziki

0

Wiki kadhaa zilizopita msanii Nassir Vanillah aliamua kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi aitwae Fatma na kuwafanya mashabiki wake wakijiuliza kuwa muziki ndio basi.

nassir1

Akiongea na Zenji255 Nassir amesema kuwa kuna baadhi ya wasanii wanaogopa kuoa wakidhani watashuka kimziki kwa sababu wanaona majukumu ya ndoa ni makubwa na kutawafanya wasifanye muziki.

“Kwa mfano Diamond na Zari japo bado hawajaoana lakini wanaishi kama mtu na mkewe na hadi leo Diamond anafanya vizuri kwenye muziki wake. kwa hiyo hata mimi sitoshuka japo kuna majukumu yataongezeka lakini naweza kubaki kwenye nafasi yangu vizuri” amesema Nassir.

Nassir amewaahidi mashabiki wake kuwa anatarajia kuachia wimbo mpya pamoja na video hivi karibuni.