Nassir Vanillah adai kuibiwa wimbo wake wa ‘DOBI’ na AT

0
nassir vanillah

Na Mkali Nesta

Sakata la ngoma mbili mpya za wasanii AT na Nassir Vanillah zinazofanana majina (Dobi) linazidi kutake over baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Zanzibar, Nassir Vanillah kulalamika kuibiwa wimbo wake wa ‘Dobi’ na AT na vile vile akaongezea kusema kuwa amepania kumshusha kimuziki.

Akizungumza na Zenji255 Jumanne, Mei 3, Nassir Wavanila amedai “Unajua kwa sasa hivi lazima wao wataongea hivyo kwasababu wamepania kunishusha kimziki mtu kama Fraga ndie aliekua producer wakati mimi naweka vocal, na nilikua nawatumia pesa ili waweze kunitumia nyimbo yangu ya dobi lakini cha kushangaza fraga amezifuta vocal zangu na kuweka za kwake na nyimbo yangu wakaimba wao.”

Katika hatua nyingine inasemekana alikuwa hajamaliza malipo kamili ya wimbo huo wakati alipourekodi lakini Nassir amesema yeye na AT walishamalizana kwasababu alimlipa pesa yake. “Nashangaa kuona AT ameachia ngoma ile ile ambayo nimeachia mimi wiki moja iliopita, yeye nyimbo kaiuza. Ilikua haina haja ya kuuza angeimba tu mwenyewe mimi sitaki niwaongelee sana ila chenye ubora kitajulikana na mashabiki ” Nassir Alimalizia.

Nimekuwekea baadhi mazungumzo ya Nassir Vanillah ambayo aliyokuwa akiongea na AT pamoja na Fraga kwa wakati tofauti.

nassir 2

nassir1