Nasikitika nafanya kazi kubwa lakini ‘Support’ inakuwa ndogo – Alatish Mabawa

0

Na Mkali Nesta

Mkali wa tungo tamu anaetokea Zanzibar, Alatish Mabawa  amefunguka yanayohusu katika muziki wake ya kuwa ‘support’ kwa upand wake kimuziki bado ni ndogo na inampa wakati mgumu kwa yeye mwenyewe. Akizungumza na Zenji255 alisema kuwa “kiukweli najitahidi kukaza buti lakini nahisi kuna mtu analegeza nyuzi za viatu vyangu. Unajua mimi sina ugomvi na wala sina beef na mtu nasikitika nafanya kazi kubwa lakini support inakua ndogo baadhi ya sehemu sijui kitu gani labda ‘some time’ binadamu anazaliwa hivyo anakua na nyota mbaya kwa watu lakini kinachonipa moyo nikwamba raia bado wanaimani kubwa na mimi kutokana na huduma ninazozitoa wanazielewa ndio maana sikati tamaa” Kuhusiana na wimbo wake mpya uitwao Woro woro, Mabawa amesema ijumaa hii anatarajia kuachia wimbo huo ukiambatana na uzinduzi wa video ya nyimbo hiyo Kwa upande mwingine alatish aliwataka watangazaji pamoja na maDj kuzitangaza kazi za nyumbani na kuwafanya mashabiki wawe na imani na mziki wao.