Nashukuru ‘My wife to be’ mashabiki wameipokea vizuri – Huza Black

0

Kwa mwaka jana 2015 aliweza kupata tuzo ya mwana Hip Hop bora. Huza Black rapper kutoka visiwani Zanzibar ambaye hana muda mrefu sana tokea aanze kufahamika lakini sasa hivi yupo katika daraja la juu katika rappers wanaofanya vizuri hapa zanzibar.

huza

Mwezi uliopita Huza aliachia wimbo wake uitwao ‘My wife to be’ na ndani ya wimbo huo akiwa amemshirikisha Smile (Kichefuchefu) ambapo wimbo huo ulitengenezwa katika studio za Most Want ed na producer Bab Chidy.

¬†Akiongea na Zenji255, Huzablack amesema anamshukuru mungu kwasababu hajategemea kama wimbo huo utaelewaka mapema. “kiukweli watu wameupokea vizuri sana wimbo wangu huu wa my wife to be kila siku zikienda mbele watu wanazidi kuelewa kilichoimbwa mule ndani”. Huza B pia alizungumzia kuhusiana na mipango ya video ya wimbo huo na kusema kuwa mipango ya video ipo njiani na amefanya na anategemea kampuni ya Bahati Entertaiment.

Na Mkali Nesta