Nakumbuka nilikuwa nashinda studio wakati natengeneza wimbo wangu wa kwanza – Didah

0

Na Mkali Nesta

Msanii wa mziki wa kizazi kipya kutoka Zanzibar Didah, amezungumzia kipindi alipokua anamzuka wa kutaka kurecord ngoma yake ya kwanza alikua anashinda katika studio ya jupiter record alifunguka hayo ijumaa hii kupitia mahojiano na Zenji255 Didah alisema “Nikisikia wimbo wangu wa kwanza uitwao hawana jipya ambao nilifanya na Aloneym nakumbuka nilipokua nashinda studio kila siku asubuhi mpaka jioni.” Staa huyo anaetamba na wimbo wa kanipase ambao unafanya vizuri katika vituo vya redio Zanzibar Didah aliongezea kuhusiana na video ya wimbo wake huo wa kanipase amesema tayari ameshashoot lakini hawezi kuwaahidi mashabiki lini itatoka kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake. Kwa mara nyingi au asilimia nyingi wasanii huwa hawapendi kuelezea kuhusiana na uandishi wa nyimbo zao lakini kwa upande wa Didah yeye ilikuwa ni tofauti, Didah alisema¬†yupo tayari kuandikiwa nyimbo na hawezi kumficha mtu atakae muandikia kama wasanii wengine wanavyokua waoga kuwataja watu walio andika nyimbo zao “kwa upande wangu mimi siwezi kumficha msanii alieniandikia nyimbo kama wimbo wangu wa lawama kandika h bizo na kama kuna msanii yoyote anataka kuniandikia mimi nipo tayari.” Kwa kipindi kirefu Didah alikuwa kimya kutokana na majukumu mbalimbali ukiachilia ya muziki anaofanya. Jikumbushie na video ya wimbo wake wa mwanzo wa Didah ambao alishirikiana na producer wa wimbo huo Aloneym, video imeongozwa na Amstrong Daddy.