Mzee Bakari aomba vyombo vya habari kuandaa matamasha ili kuusaidia muziki wa Zanzibar

0

Meneja wa studio ya Action Music iliyopo visiwani Zanzibar Mzee Bakari Shomari ameviomba vyombo vya habari kuwasaidia wasanii wa Zanzibar katika kuandaa matamasha mingi ya muziki ili kuunyanyua muziki wa Zanzibar.

mzee bakari
Mzee Bakari Shomari akipeana mkono na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein

Akizungumza na Zenji255 Mzee Bakari Shomari amesema kuwa vyombo vya habari vinatakiwa kuwa na umoja na kufanya kitu kwa pamoja kwani Zanzibar wapo wasanii wengi na wazuri.

“Zanziba tunayo matamasha lakini hayatoshi, Zamani kulikuwa kuna taasisi mbali mbali zikiandaa matamasha ila siku hizi mambo haya yamepungua. Nakumbuka redio zetu zilikuwa zinashirikiana na kuungana na kufanya matamasha na watu walikuwa wanakuja wengi tu. Sasa kwanini hili jambo lisirudi na kwa asilimia nyingi  litaingiza faida kwa wahusika wote kuanzia redio husika, wasanii, jamii na serikali kwa ujumla” Amesema Mzee Bakari.

Injinia Bakari Shomari vile vile ameongezea kuwa kipindi yupo East African Melody Taarab redio ya Clouds FM iliwasaidia kundi hilo kwa kuwaalika katika matamasha mbali mbali yaliyofanyika Dar es Salaam na kuwafanya kundi hilo kuwa maarufu mpaka sasa.