‘Muziki sio sababu ndoa yangu kufikia hapa leo’ – Nassir Vanillah

0

Msanii Nassir Vanillah hivi karibuni baada ya kuachia kava ya wimbo wake ‘Najuta Kuoa’ anaotarajia kuuachia ambapo jina la wimbo limezua utata mkubwa na maswali mengi kwa mashabiki wake.

nassir

Akizungumza na Zenji255 Nassir amesema kuwa muziki wake hauwezi kuwa sababu ya ndoa yake kuwa na matatizo kwani hakuna mtu asiyemfahamu kama yeye ni msanii.

“Watu wote mpaka familia yangu inafahamu kama mimi nafanya muziki na matatizo katika ndoa yapo kila sehemu ila kwa upande wangu mimi siwezi sema kama ndoa yangu ndio basi tena, hapana, ila ipo katika hali ambayo si ya kusema kwa sasa.” Amesema Nassir Vanillah.