Mubacriss azungumzia kuhusiana na serikali kuibua vipaji vya muziki mashuleni

0

Hitmaker wa wimbo wa mapenzi mkoleni, Mubacriss amesema kuwa amependa maazimio yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud kushirikiana na waziri wa Elimu pamoja na Baraza la Sanaa Zanzibar yanayohusiana na kuibua vipaji vya muziki mashuleni.

mubacriss

Akizungumza na Zenji255 Mubacriss amesema kuwa kwa hapo mwanzo wakati ulikuwa bado ila anaamini kama serikali itaamua kulishikilia na kuliweka msisitizo basi tutafanikiwa.

“Maneno aliyoyasema Mkuu wa Mkoa na wakishirikiana wizara ya Elimu yatafanyiwa kazi kiukweli Zanzibar itafika mbali katika kuibua vipaji mashuleni, kwani kuna ndugu zetu wengi wana vipaji lakini inashindikana kuviendeleza vipaji vyao.” Amesema “Serikali ina uwezo mkubwa wa kuyashawishi makampuni makubwa makubwa kusaidia shughuli kama hizi za kuibua vipaji kuanzia shule za msingi mpaka sekondari, kwa uwezo wa mungu kila kitu kinawezekana.” Alimalizia Mubacriss.