Categories
E! News

‘Mtangazaji alitaka elfu 20 kama ada ya kunifanyia mahojiano kwenye redio’ – Harmo Music

Msanii anayechipukia wa muziki kizazi kipya, Harmo Music amesema alitakiwa alipe elfu 20 kwa ajili ya kupewa nafasi ya kuutambulisha wimbo wake mpya pamoja na kufanyiwa mahojiano katika kituo hicho cha redio.

harmo music

Akiongea na Zenji255 amesema kuwa siku ya kwanza wakati wimbo wake anaupeleka katika vituo vya redio kuna baadhi yao walikubali kuucheza ila kuna baadhi walitaka awalipe kiasi kadhaa kwa ajili ya ya kuutambulisha wimbo huo.

“Vituo viwili viliniambia maneno tofauti, mmoja, alisema anataka nimpe elfu 20 atanifanyia mahojiano na kuutambulisha wimbo. wapili, aliniambia maneno hayo hayo lakini alizidisha kiwango, alitaka elfu 40 lakini ni kuutambulisha wimbo tu” Amesema Harmo Music.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.