Msichana asiye na mikono ashinda tuzo ya muandiko bora

0
msichana

Msichana wa miaka saba aliyezaliwa bila mikono ameshinda shindano la muandiko mzuri nchini Marekani. Anaya Ellick kutoka Chesapeake,Virginia hatumii viungo vya kumsaidia wakati anapoandika.

Wakati anapoandika yeye husimama huku akishikilia kalamu yake katika mikono. Mwalimu wake mkuu Tracy Cox kutoka shule ya Greenbrier Christian amemtaja kuwa mtu wa mfano mwema.

”Yeye uhakikisha kuwa hakuna kitu kinachomzuia kufanya atakalo”,alisema Cox.”Ni mkakamavu na ana muandiko mzuri katika darasa lake”.

Msichana huyo anadaiwa kuwashinda washindani wengine 50 ili kushinda taji hilo la kitaifa. Orodha hiyo ya tuzo huwazawadi wanafunzi wenye akili, matatizo ya kimwili, au ulemavu endelevu.

Source: BBC Swahili