Mshindi wa Free Style Chiby K aingia studio kurekodi wimbo wake mpya

0

Mshindi wa shindano la Run The Beat Free styke Battle, Chiby K ameonekana hapo jana Jumatatu katika studio za Mandevu records akitayarisha wimbo mpya ikiwa kama ni moja ya makubaliano kwa mshindi wa shindano hilo.

Chiby K (Kulia) akiwa na Mtayarishaji wa Mandevu records, Buju (katikati) pamoja na MC Kudo (Kushoto)

Hivi karibuni Chiby K aliibuka mshindi wa shindano hilo baada ya kumbwaga mpinzani wake ‘Devil’ ambaye aliyetoka nae toka awamu ya mwanzo na kumshinda katika hatua ya fainali. Ambapo mshindi anajipatia nafasi ya kurekodi wimbo mmoja kutoka studio ya Mandevu na Video moja kutoka kwa director Huruma.

chiby k

Akiongea na Zenji255, Chiby K amesema kuwa nafasi aliyoshinda ataitendea haki kuanzia wimbo hadi video kwani anataka kudhihirisha kama yeye kweli alikuwa ni mshindi mstahiki katika mashindano hayo.

“Wimbo ndio tayari upo jikoni unaanza kuwekwa viungo na mambo mengine, vile vile mipango ya video itafuata baada ya mimi kuwa tayari nishaweka sauti na kila kitu halafu kabla ya wimbo kuisha nitachukua demo kwa ajili ya kurekodi video na baadae wimbo utawekwa ukiwa tayari, cha zaidi ninachowaomba mashabiki wa muziki wanipokee kijana wao Chiby K Solja” Amesema Chiby K