Msanii Chidy Yobo kufuata nyayo za Pozi Adimu

0
chidy

 

Msanii chipukizi kutokea visiwani Zanzibar ambae anafanya vizuri kwa sasa, kwenye Radio na Televishen za visiwani humo, ameamua kufuata nyayo za Msanii mkongwe na Maarufu Zanzibar Pozi Adim.

Akipiga stori na PaparaziMzenji Chidy alisema ”Pozi Adim ni msanii mkubwa hapa zanzibar na sote mimi na yeye tunatokea Managment moja ya Goodfather Music Entertainment inayo simamiwa na mameneja wawili IMA MI8 na Khamis Hk(Kaka Meneja), licha kua tupo wote lakini namuona Pozi ni mtu wa kujituma sana, na mara nyengine nashuhudia akitafuta connection nje ya Zanzibar kwa Faida ya kwetu sote na Management.”

image
Chidy aliongea kuwa “Kwahiyo¬†na mm nimeamua sitaki kua mzigo tuu unaobebwa, kwa sasa nataka kua msaada pia wa managment yangu katika kutafuta connection za nje ya kisiwa cha Zanzibar.” Alipoulizwa ni kwa namna gani anaweza kupata connection nje ya Zanzibar na connection zake zitasaidia nini katika uongozi wake, Chidy alisema
Hiv sasa anaandaa safari ya Dar, licha ya kua ni safar ya shughuli nyengine za kifamilia lakini atahakikisha hapotezi chance yoyote ile ya kujitangaza pamoja na kutangaza mziki wa nyumbani Zanzibar.
”Unajua msanii na wewe ukiwa unajituma katika kujibrand inaipunguzia mzingo Managment yako, na inakua ni rahisi kufikia malengo kwa haraka kuliko kila kuachia management peke yake hasa ukizingatia bado management yetu ni changa kwa upande wa pili wa Muungano, tunaomba Mashabuki watuunge mkono kwa hili na kutuombea” Alimalizia Chidy Yobo.