Mo Fire azitaja nyimbo za wasanii wa Zanzibar katika studio yake

0

Mtayarishaji kutokea studio ya Mo Fire, Producer Mo Fire amezitaja nyimbo za wasanii wa Zanzibar ambazo wasanii mbali mbali kutokea Zanzibar wametengeneza katika studio yake.

mo fire

Mo Fire amewataja wasanii hao ni Chaby Six, Alpha (Nikatae), Warda (Naishi nao), Job Fire ( Salama) na Roja King.

Akizungumza na Zenji255 Mo Fire anasema kuwa “Kwa mimi na wasanii wa Zanzibar ni kama ndugu zangu tena huwa nawapa kipaumbele wanapokuja kufanya kazi katika studio yangu, unajua mtu yupo sehemu tofauti na mimi nilipo na ameondoka mbali na nyumbani.”

“Mimi nitakuwa mstari wa mbele kuwasapoti wasanii wa Zanzibar kwa sababu nataka kuona msanii japo mmoja wa huko (Zanzibar) kuisimamia na kuitambulisha nchi yetu sehem yoyote ile kama wasanii wengine” aliongezea Mo fire