‘Mimi huwa nafurahia sana ninapowasimamia vijana kwenye muziki hata kama sipati faida’ – Khamis HK

0

Kuna watu wengi wanajaribu kuwasimamia wasanii lakini wanaishia njiani kutokana kusema hakuna faida katika muziki wa Zanzibar.

khamis HKZenji255 ilizungumza na Meneja kijana kutoka Zanzibar Khamis HK amesema watu wanaoamua kujitolea kumsimamia msanii wengi wao huwa wanaweka malengo kitu gani watapata baadae lakini hawafanyi kama vile vitu wanavipenda kutoka moyoni mwa na wanataka kuwanyanyua wasanii hata kama hawatopata faida.

“Mimi sitojali kama nimepoteza muda wangu kutokana na kuwasaidia wasanii wa Zanzibar, muziki wetu haujafikia hatua ya kuweka malengo utapata nini baadae ila muziki wetu ni wa kujitolea sana. Ukiamua kufanya kazi yoyote kwanza unatakiwa uipende kazi yako usijilazimishe na wala usilazimishwe na mtu kinyume na hapo utaishia njiani tu kwa mfano mimi ninaipenda kazi yangu na nafurahia sana nikiona Zanzibar wasanii wanakuwa wengi kila siku na wanafanya vizuri” Alisema HK.