Mfahamu mzee Laiboni ana watoto 70 na wajukuu 300 Tanzania

0

Nchini Tanzania katika mkoa wa Arusha wilayani Monduli, mzee mwenye zaidi ya miaka 100 ana watoto zaidi ya 70 na wajukuu 300.

tanzania

Mzee Meshuko Ole Mapi, almaarufu Mzee Laibon, amelazimika kuwa na shule yake na soko kwa ajili ya jamii yake hiyo na anasema bado ana azma ya kuendelea kuoa.

Watu kutoka mataifa mbali mbali hufika kumtembelea mzee huyo kama sehemu ya utalii.

_91316084_laiboni5

Na mwandishi wa BBC Esther Namuhisa alimtembelea mzee huyo Kaskazini mwa Tanzania.

Aliwasili katika himaya ya mzee Laiboni na kuona soko linalouza vitu vya asili ambapo aliwaona kina mama na vile vile watoto wengi tu,na kufanikiwa kuzungumza na baadhi ya wanawake hao.

_91316082_laiboni6

Mwanamke mmoja anayeuza vitu vya watalii kama bangili na shanga, alimwelezea kwamba soko hilo linaundwa na wanafamilia wa mzee Laibon,na si la kawaida kama yalivyo masoko mengine,kwa sababu bidhaa zinazouzwa hapo,wateja wake huwa watalii wanaoshangazwa na maajabu ya mzee Laiboni kuwa na watoto 70 na wajukuu 300,licha na kuwa na wake wachache.

Katika eneo hilo mwandishi huyo aliona nyumba zaidi ya arobaini hivi,na chini ya mti mmoja akakutana na mzee Laiboni ambaye amepumzika.

Alimuuliza idadi ya familia yake na shule aliyoanzisha na kwa sababu mzee huyo hajui lugha ya kiswahili alikuwa na mkalimani wake ambaye alimtafsiria lugha ya kiswahili.

_91316087_laiboni4

Mkalimani wake alisema kuwa mzee Laiboni ana wake wanane na takriban watoto sabini na sita mbali na wajukuu karibu mia tatu.

Kuhusu ni vipi angeweza kuhudumia familia yote hiyo licha ya umri wake alisema kwamba,wakati wa kiangazi yeye huuza ngombe na kununua mahindi.

Aliongezea kuwa idadi ya ng’ombe alionao inakaribia 3000.

Mzee laiboni alisema kuwa wazo la ujenzi wa shule,lilijiri kwa sababu watoto wake walikua wanasoma shule ya mbali na kuna wakati walikua wakishindwa kwenda shule kutokana na tembo ambao pia waliwahi kuua mtu.

_91316089_laiboni2

Baadaye mwandishi huyo alizuru shule ya mzee Laiboni ambapo alikutana na mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Mwalimu huyo alisema kuwa licha ya kuwa mzee Laiboni sio mbaguzi ijapokuwa asilimia 90 ya wanafunzi wote ni watoto wake.

Kwa hisani ya: BBC Swahili