Mfahamu Lady Black: Rapa wa kike pekee kutoka Zanzibar aliyevutiwa na Sista P

0

Katika kiwanda cha muziki ambacho kina rappers wa kike wachache kutoka Zanzibar, Lady Black kwa kipindi kirefu alikuwa kimya na sasa amerudi tena rasmi baada ya kuonekana studio za Action records akiwa anaanda midundo mipya kutoka studio hapo.

Lady Black akitoa free style katika show ya mualiko wa chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya iliyofanyika Coco Blue – Jambiani.

Huenda ukawa unamfahamu juu juu tu, mfaham zaidi.

Kwa jina kamili anaitwa Felista Philipo Magindo a.k.a Lady Black kwa sasa makazi yake ni Zanzibar, alianza sanaa ya muziki wa rap miaka saba iliyopita ambapo alikuwa akirap akiwa kwenye Ma-Camp (kwenye mkusanyiko). Kwa kipindi hicho alikuwa bado hajapata nafasi ya kuingia studio kwani kwa upande wake anasema hali ilikuwa ngumu kwenda studio.

“Yaani katika huwezi kuamini nilianza kuingia studio miaka miwili iliyopita katika saba ya muziki wangu. Na wasanii walionivutia zaidi na kunifanya mpaka nikaupenda muziki hasa hasa rap: Sista P, Zay B na Witness. Na kwa sasa tayari nilishaachia nyimbo 2, na nyingine tayari ipo jikoni inasimamiwa na producer Chilly K wa Action records” Amesema Lady Black.

Ameongeza kuwa katika kilichokuwa kinamfurahisha katika muziki na sehemu aliyokuwa anaishi Kigamboni, kulikuwa na ushindani mkubwa wa ma-Camp ambapo wanashindanishwa kurap (Free style Battle) na yeye ndipo akaamua kujiingiza katika mashindano lakini hakufanikiwa kushinda ila haikumfanya akate tamaa kwenye rap.

“Kwa kweli bado natamani mashindano yale ya ma-Camp yarudi tena hata huku Zanzibar¬† yawe yanafanyika kila mwezi au kila baada ya miezi kadhaa yafanyike sababu yanaibua vipaji vingi ila watu hawajui” Amemalizia Lady Black.