Meek Mill ahukumiwa miezi 3 kifungo cha ndani ya nyumba

0

Meek Mill hatoenda jela lakini hatokuwa huru pia. Siku ya Ijumaa (Feb 5) hakimu aliyesimamia kesi ya rapa huyo kutokea Philadelphia aliamuru atumikie kifungo cha miezi 3 akiwa nyumbani kwake kutokana na kesi inayomkabili.

Mtandao wa TMZ ulieleza kuwa, Meek Mill hukumu hiyo aliyopewa ya kutumikia siku 90, atashindwa kufanya show zake, kutengeneza nyimbo mpya na wala kutengeneza nyimbo za uchokozi. Vile vile hakimu Genece Brinkley aliongezea hukumu nyingine ya kukaa katika kifungo cha majaribio kwa muda wa miaka sita.