‘Mchongo wa kufanya kazi na Koffi Olomide kuna watu walinibania – AT

0

Muimbaji wa Mduara kutoka visiwani Zanzibar, AT anaamini ili muziki wa Tanzania ukue lazima kuwe na umoja na unafiki uishe.

image

AT amesema watu wenye roho mbaya wamejaa kwenye muziki wa Tanzania. Akiongea na Zenji255 AT amesema kuna mchongo aliowahi kuupata wa kufanya kazi na msanii wa DRC, Koffie Olomide lakini kuna watu walimbania ikashindikana.

“Nilikuwa na mchongo wa kufanya kazi na Koffi Olomide watu niliyowafuata wakanitosa kwa kuhofia wasanii wao watashuka. Wapo wenyewe wanajijua kabisa niliwafuata na wakaniyeyusha na mimi nawajua ni kitu ambacho huwa kinaniuma sana. Ndio maana leo nimeamua kusema ila wajue tu kuwa shetani huwa hafungwi jela,” amesema AT.

Source: Bongo5