“Mbio za magari kwangu ni muhimu kuliko mpira wa Chelsea na Arsenal” – Jose Mourinho

0

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amewashangaza wengi baada ya kuacha kwenda kutazama fainali ya FA Cup kati ya Arsenal na Chelsea katika uwanja wa Wembley nchini Uingereza.

mourinho

Kocha huyo ambaye ametoka kutwaa taji la ligi ya Europa kwa mara ya kwanza akiwa na United, ameonyesha kuwa na misimamo yake binafsi baada ya kuacha fainali hiyo ya FA na kutimkia jijini Monaco katika fainali za magari maarufu kama Formula One.

Inasemekana Mourinho alipata mualiko wa kuhudhuria fainali hizo za Formula One kutoka kwa timu ya REDBULL ili kupata nafasi ya kuwatazama waendesha magari wa timu hiyo Max Verstappen na Daniel.

Ikumbukwe kwamba kocha Jose Mourinho baada ya kufanikiwa kubeba kombe la Europa alitoa tamko kwamba “Sitajihusisha na mpira ndani ya mwezi mmoja na najua kwamba leo kuna fainali ya FA, lakini pia Ujerumani kuna fainali na hata Hispania pia, Sitaki kabisa na sina hata hamu ya kupata matokeo”

Mourinho pia aliongeza kwa kusema “Huu ndio muda muafaka wa kuacha kabisa kufikiria mpira na kufanya mambo mengine, kuwa karibu na familia na marafiki ili nisahau mpira kwa sasa nataka iwe hivyo”