Mbaraka Said Husun achaguliwa kuwa mwenyekiti wa Michezo katika ofisi ya makamu wa pili wa Rais

0

Kamati ya Michezo ya Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais leo imefanya uchaguzi wa kuchagua Mwenyekiti na Makamo Mwenyeti wa kamati hiyo inasimamia michezo mbali mbali katika Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais ikiwemo Mpira wa Miguu, Netball, Volball, Handball na Basketball, ambapo uchaguzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani ikiwa ni hatua ya kuchagua viongozi wapya baada viongozi waliokuwepo kumaliza mda wao wa kuongoza Miaka mitatu.

uchaguzi

Nafasi ya Mwenyekiti imegombaniwa na Said Issa Kirobo Kutokea Idara Uendeshaji na Utumishi na Mbaraka Said Husun kutokea Tume ya Uchaguzi Zanzibar. Huku nafasi ya Makamo Mwenyekiti hakuweza kujitokeza mtu yoyote hivyo mshindi wa kwanza amekuwa Mwenyekiti na wapili amekuwa makamo Mwenyekiti.

Kwa upande wa Matokeo ya Uchaguzi huo, Mbaraka Said Husun kutokea Tume ya Uchaguzi Zanzibar aliibuka mshindi baada ya kupata kura 168 huku mpizani wake Said Issa Kirobo Kutokea Idara Uendeshaji na Utumishi akiibuka na kura 53, ambapo jumla ya kura 222 zilipigwa na 1 kuharibika.

Imetayarishwa na:Ali Khamis (Prince Almecky)