Mash Marley azungumzia ujio mpya wa Kilinge cha Hip Hop Zanzibar

0

Je Unafahamu nini maana ya Kilinge? Hivi karibuni meneja anaemsimamia rapa Ison Mistari, Mash Marley amesema yuko katika harakati za kuanzisha Kilinge ambacho kitakuwa kinakusanya na kuwaweka pamoja vijana wenye vipaji vya ‘kuchana’ mitindo huru (free style) ambapo itakuwa ikifanyika kila mwezi hapa Zanzibar.

mash marley

Akiongea na Zenji255 Mash amesema kuwa wakati alipokuwa katika akifanya ziara ya kusambaza video ya Ison Mistari ‘Nani Nilimkosea’ katika vyombo mbali mbali vya habari, alisoma vitu vingi kupitia ziara hiyo ikiwemo umoja wa wasanii wa Hip Hop katika jiji hilo ambao huwa kila jumamosi hukutana na kufanya mashindano ya mitindo huru katika kilinge chao kijulikanacho kama Tamaduni Music.

“Mimi ziara yangu ya kwenda bongo sikwenda kwa sababu ya Ison nilienda kwa sababu kukusanya mawazo mapya kwa ajili ya muziki wa Zanzibar, Na niliona ni vizuri hiki kilinge tukikileta huku Zanzibar ili tuweze kupata vipaji vipya vya Hip Hop kila mwezi. Na kila kitu tayari nishamaliza mazungumzo na baadhi ya wana Hip Hop bongo watakuwa wanakuja kutoa darasa katika kila kilinge kinapofanyika” Amesema Marley.

Ameongezea Mash kuwa kati ya wasanii alioweza kuongea nao na kukubali kuwa watakuja kwenye kilinge kitakapoanza ni kama One the Incredible, KBC (Kwanza Unit) Nikki mbishi, Wakazi na wengine wengi.