Mapenzi hata kwa wasanii wa HIP HOP yapo, Barua ya mapenzi ya Tupac Shakur aliyomwandikia Msichana Inauzwa kwa $35,000

0

Kuna baadhi ya misemo ya vijana wa sasa husema kuwa “Sio wasanii wanaobana tu pua hulia na mapenzi kwenye nyimbo zao bali hata wana HIP HOP nao wamo.”

Barua ya mapenzi ya Tupac Shakur ipo mnadani inauzwa na  msichana ambaye aliyekuwa akisoma nae darasa moja mwaka 1988 na ndiye anaeiuza barua hiyo kwa dola 35,000 sawa na Milioni  73,500,000 za kitanzania, ambapo anaiuza kupitia madalali  wanaouza vitu vya kumbukumbu.

Kupitia mtandao wa TMZ, Msichana huyo alipewa jina la utani na Tupac la ‘Beethoveen’ kwa sababu alikuwa anapiga chombo cha muziki aina ya piano. Kwa maneno ya hisia aliyoyaandika Tupac kwenye barua ambayo yalionekana ni ya kiufundi na yenye upendo wa hali ya juu kwa msichana ambayo yaliyoandikwa kwa mkono wa Tupac mwenyewe. “Nadhani utakuja kugundua hivi karibuni, na wala sitosema maneno ya kiburi.” Aliandika Tupac “Hivyo kama kuna kitu nimesema na kimekutisha, tafadhali usiwe na hofu kwa sababu hisia zangu zimepitiliza kwako”

Pia msichana huyo alielezea uhusiano wao ulivyokuwa na Tupac “Sikuweza kumjua kijana ambaye aliyechora tatoo iliyoandikwa THUG LIFE katika kifua chake na aliyekufa kwa kupigwa risasi katika mitaa ya Las Vegas.” alisema ” Pia sikuweka maanani juu ya muziki aliyokuwa akirekodi, ilikuwa haina kitu kama vile alivyokuwa akifanya ‘Mawazo Huru’ (Freestyles) katika shule yetu.”

Tupac Alifariki kwa kupigwa risasi mnamo Septemba 13, 1996 na akiwa na miaka 25.