Mantuzzo azungumzia kuhusu ukimya wake na ujio wake mpya

0

Kwa muda mrefu msanii Mantuzzo ameonekana kuwa kimya katika sanaa yake ya muziki, na vile vile amezungumzia kuhusiana na ujio wake mpya baada ya ukimya huo.

mantuzzo

Akizungumza na Zenji255 Mantuzzo amesema kuwa aliamua kukaa kimya kutokana na mambo ya maisha na muziki wake na ndio akaamua kutulia ili kuangalia wapi alipokosea ili arudi katika kasi ya kimaajabu.

“Muziki bado nafanya na kazi zipo jikoni na ndio kitu ambacho kwa sasa kinaniweka kimya muda mrefu kwani nahangaika kila sehemu kuweka mambo sawa hata nikirudi nirudi kwa kishindo cha kuwastaajabisha mashabiki” Amesema Mantuzzo.

Ameongezea kuwa “Kwa sasa maandalizi ya wimbo na video yake tayari kuna kazi nimefanya na Ison, studio ya Stone Town Records na inawezekana video nitafanya hapo hapo. Vile vile nina wimbo ulitoyarishwa na Bonge Jr. na nyingine karibuni nitatoa taarifa.”