Categories
E! News

Mantuzzo asema uwezo wake wa kufanya video ni Milioni 5

Ukitaka kutengeneza video kali, zenye viwango vya kimataifa ni lazima ugharamike pesa nyingi sana. Kuna baadhi ya wasanii kwao wao huwa ni ngumu sana kuzimudu gharama hizo.

mantuzzo

Msanii Mantuzzo anasema kuwa anapenda kufanya video nzuri zenye soko la kimataifa iliĀ  muziki wake ukue lakini gharama zake ni kubwa kwani kwake yeye kiwango chake cha mwisho ni shilingi Milioni 5.

Akizungumza na Zenji255 Mantuzzo anasema “Changamoto kubwa kwangu ni kuwa na pesa ya kutosha, kwa sababu ninaweza nikawa na pesa lakini je inaweza ikakidhi mahitaji ya soko ambalo lipo kwa sasa? Napenda nifanye video za viwango vya juu lakini uwezo wangu wa kufanya video ni chini ya Milioni 5.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.