Man Chado kuja na ‘Kwa ajili ya wana’ akiwa na Juma Nature

0

Rapa wa muziki aliyekaa kimya kwa muda mrefu kutokea kundi la Murder Squad, Man Chado maarufu alikuwa akijulikana kama Chadogi. Anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaoitwa “Kwa Ajili ya Wana” akiwa kama ‘Solo’ ambapo katika wimbo huo amemshirikisha Juma Nature.

man chado

Akizungumza na Zenji255 Man Chado amesema kuwa, ukimya wake wa muda mrefu alikuwa akijiweka sawa kimaisha pamoja na kuusoma muziki na mabadiliko yake. Man Chado alikuwa ni mmoja ya wasanii wa muziki wanaounda kundi la Murder Squad ambapo mwaka 2007 aliamua kujiengua kwa ajili kufanya shughuli nyingine za kimaisha.

“Nimeamua kuubadili muziki wangu ili kuwaonjesha ladha nyingine wana wangu, kwani wimbo upo tayari na umetayarishwa katika studio za Mandevu chini ya wapishi wawili Lummie na Buju. Na ndani ya wimbo nimemshirikisha mkongwe Juma Nature na wimbo utakuwa masikioni mwa wana karibuni tu, wakae mkao wa kuupokea wana”