Mambo na vijimambo: Unajua kunguni huwa wanapenda rangi gani?

0
kunguni

Watafiti nchini Marekani wanasema wamegundua kunguni hupenga baadhi ya rangi kushinda rangi nyingine. Watafiti hao, baada ya kufanya uchunguzi wa kina, wanasema kunguni hupenda sana rangi zilizokosa. Sana, wanapenda rangi nyeusi na rangi nyekundu.

Hata hivyo, huchukizwa sana na rangi ya manjano na rangi ya kijani kibichi. Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la Journal of Medical Entomology. Matokeo hayo yanaweza kusaidia watu kuwatega na kuwanasa kwa urahisi wadudu hao. Hata hivyo wanasayansi hao wanasema bado ni mapema kubaini iwapo shiti za rangi ya manjano zinaweza kutumiwa kuwafukuza wadudu hao kitandani.

Kunguni ni wadudu wadogo sana na hutaka kukaa karibu sana na chakula chao, damu yangu. Wanaweza kujificha katika godoro, nguo na mianya kitandani. Hupenda pia vitambaa na mbao badala ya plastiki na chuma.

Lakini Dkt Corraine McNeill na wenzake walitaka kubaini iwapo rangi zinaweza kuathiri maeneo wanayovamia.

colors

Walitumia vibanda vidogo vya rangi mbalimbali kwenye maabara na kuchunguza kungini walipenda kujificha wapi. Walioneana kupenda kujificha katika rangi zilizofanana na miili yao, rangi nyeusi na nyekundu. Daktari huyo anasema awali walidhani kunguni wangependelea rangi nyekundu kwa sababu damu ni ya rangi nyekundu.

“Hata hivyo, baada ya uchunguzi, sababu kuu tuliyobaini iliwafanya kupenda rangi nyekundu ni kwa sababu kunguni hao wenyewe huonekana wakiwa wa rangi nyekundu, hivyo hudhani rangi hiyo ni kunguni wenzao.” Huchukia rangi ya manjano na rangi ya kijani kibichi kwa sababu rangi hizi za kung’aa huwakumbusha kuhusu maeneo yenye mwanga ambayo huwa si salama kujificha.

Utafiti uliofanywa awali umebainisha kwamba rangi hizi huwa pia hazipendwi na wadudu wengine wafyonza damu kama vile mbu.

CHanzo: BBC Swahili