Mama mzazi wa Tupac, Afeni Shakur amefariki dunia akiwa na miaka 69

1
afeni shakur

Aliyeakuwa mwanaharakati katika kundi lililokuwa likitetea haki za watu weusi (Black Panther) nchini Marekani Afeni Shakur, na pia ni mama mzazi wa hayati Tupac Shakur amefariki dunia. Alikuwa na miaka 69.

Afeni Shakur alifariki akiwa hospitalini ambapo ilisemekana mnamo majira ya saa 3:43 Usiku alisafirishwa kutoka nyumbani kwake baada ya kupata mshtuko wa moyo na kuwahishwa hospitali ambayo iliyokuwa karibu na eneo analoishi, Lakini usiku huo wa Jumatatu (May 2) saa 10:28 ilipokelewa taarifa kuwa amefariki.

Akiwa kama muanzilishi na kiongozi, Afeni alisimamia mashirika mbali mbali ya mwanawe kama Tupac Amaru Shakur Foundation, ambayo yalifunguliwa baada ya kifo cha Tupac mnamo mwaka 1996. Tupac Aliuliwa kwa kupigwa risasi mjini Las Vegas.

Afeni pia alikuwa ni mlinzi wa mali za Tupac, na katika majukumu hayo alisimamia albamu za mwanawe na Filamu ya All Eyes on Me inayotarajiwa kutoka miezi ya hivi karibuni ambayo inayoeleza maisha ya mwanawe Tupac tokea utotoni kwake mpaka kufanikiwa katika muziki.

Tupac alishawahi tengeneza baadhi nyimbo zinazomuhusu mama yake, na iliyopata maarufu zaidi ni ‘Dear Mama’ wimbo uliyokuwa ukieleza maisha ya tabu aliyoipata mama yake akiwa jela kwa kuhusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya.

Inaaminika ya kuwa Afeni amefariki na mshtuko wa moyo lakini kifo chake mpaka sasa kinafanyiwa uchunguzi.

Soma baadhi ya mashairi yaliyokuwemo ndani ya wimbo wa Dear Mama na angalia video yake hapo chini.

“There are no words that can express how I feel / You never kept a secret, always stayed real / And I appreciate how you raised me / And all the extra love that you gave me / I wish I could take the pain away / If you can make it through the night, there’s a brighter day / Everything will be alright if you hold on / It’s a struggle every day, gotta roll on / And there’s no way I can pay you back / But my plan is to show you that I understand / You are appreciated.”