Makocha wa Yanga wakiperuzi Baada kazi nzito huko Pemba

0
Yanga

BAADA ya saa za kazi, walimu wa klabu ya Yanga, ambayo ipo kisiwani Pemba. Kocha Mkuu Plum na Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi, walipata muda wa kuperuzi mitandao mbali mbali, wakati walipokuwa uwanja wa Gombani Chakechake Pemba, ambapo kikosi cha Yanga kilipiga kambi kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara baina yake na Azam unaotarajiwa kupigwa Jumamosi ya tarehe 9 mwezi huu,

Mwambusi alisema wachezaji wengi wote wanaendelea vizuri na mazoezi chini yao, na kuwa wamejipanga kuhakikisha kikosi chao kinashinda katika mchezo huo.
Yanga inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kufikisha pointi 46, sawa na Azam, lakini wanapishana kwa tofauti ya magoli, imeweka kambi visiwani Pemba, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Azam FC.
(Picha na Haji Nassor, Pemba)