Makaranga kurudi na ujio wa wimbo mpya hivi karibuni

0

Msanii wa muziki wa kizazi kipya zanzibar, Makaranga amesema anatarajia kuachia wimbo mpya (jina bado) hivi karibuni baada ya ukimya mrefu wa kujipanga zaidi.

makaranga

Akiongea na Zenji255 amesema kuwa wimbo huo mpya utakuwa ni ujio wake mpya baada ya kukaa kimya kwa muda wa mwaka mzima toka aachie wimbo wake ‘nipo nawe’ mwishoni mwa mwaka 2015.

“Ukimya wangu umezua maswali mengi kwa mashabiki wangu lakini nawaambia kuwa mwezi huu nitaachia wimbo wangu mpya kesho (Januari 11) nitaanza kupost ‘cover’ ya wimbo kwenye mitandao ya kijamii” amesema Makaranga.

Kuhusiana na video ya wimbo huo amesema kuwa sasa hivi yupo tayari katika mipango ya kufanya tena video, baada ya video ya wimbo wa mwanzo kufeli kutokana na matatizo ya kimaisha na familia yaliyojitokeza.