Categories
E! News

Majina ya mapacha wa Jay Z na Beyonce yawekwa hadharani

Mtandao wa TMZ umeripoti kupatikana kwa majina ya watoto mapacha wa Beyonce na JAY-Z.

beyonce

kwa mujibu wa TMZ Watoto hawa wamepewa majina Rumi Carter Na Sir Carter na imegundulika kuwa JAY-Z na Beyonce waliyasajili majina haya mapema tu kabla ya kuwapa watoto wao ili kuweza kuzuia biashara yeyote kufunguliwa kupitia majina ya Rumi Carter na Sir Carter waliozaliwa jumatatu ya June 12-2017.

Majina haya hayata ruhusiwa kutumika kwenye biashara ya vitu kama manukato, vipodozi, vishikila mapambo ya meno ya watoto, basikeli za watoto, vikombe, chupa za maji, vibanio vya nywele, karata, mabegi, vifaa vya michezo na vitabu vya watoto.

Rumi na Sir wamejiunga na dada yao mwenye miaka mitano Blue Ivy katika familia ya The Carter.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.