Liverpool watinga robo fainal ya ligi ya Europa. (+Video)

0

Siku moja baada ya michezo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuchezwa na kushuhudia vilabu kadhaa vikiaga mashindano hayo, usiku wa April 14 ilikuwa ni zamu ya kushuhudia robo fainali ya michuano ya UEFA Europa league.

Miongoni mwa michezo iliyokuwa inatazamwa usiku wa April 14 ni mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Borrusia Dortmund uliyochezwa katika dimba la Anfield, mchezo huo ulimalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 4-3, hivyo kuiondoa Dortmund kwa aggregate ya 5-4.

image

Magoli ya Dortmund yalifungwa na Henrik Mkhitaryan dakika ya 5, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 9 na Marco Reus dakika ya 57, wakati magoli ya Liverpool yalifungwa na Divock Origi dakika ya 48, Philippe Coutinho dakika ya 66, Mamadou Sakho dakika ya 78 na Dejan Lovren dakika ya 90.

Angalia ‘Highlight’ za mechi hiyo ya Liverpool na Dortmund