Ligi Kuu Zanzibar: KMKM yaichakaza Kilimani City 2-0

0

Klabu ya Mabaharia wa KMKM jioni ya jana imefanikiwa kupata alama tatu muhimu baada ya kuifunga Kilimani City 2-0 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja uliopigwa katika Uwanja wa Amani.

kmkm

Magoli ya KMKM yamefungwa na Said Mohammed  dakika ya 24 na Mudrik Muhibu kwenye dakika ya 56 ambapo hilo ni bao lake la 9 katika ligi hiyo akiwa nafasi ya tatu kwa kufunga mabao ambapo Ibrahim Hamad Hilika wa Zimamoto anaongoza na mabao yake 11 akifuatiwa na Hakim Khamis pia wa Zimamoto mwenye mabao 10.

Matokeo mengine ya jana kwa upande wa kanda ya Pemba katika Uwanja wa FFU Finya, Okapi na Kizimbani zimetoka sare ya bila kufungana na katika Uwanja wa Gombani Chipukizi imeichapa African Kivumbi mabao 5-0.