Leicester City watangazwa rasmi mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza 2015/16

0
leicester city

Klabu ya Leicester City kwa mara ya kwanza baada ya miaka 132 katika historia wametangazwa rasmi kuwa ni mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza.

Leicester imetwaa taji hilo baada ya mechi ya timu iliyokuwa nafasi ya pili ikiwa na point 70 katika ligi hiyo, Tottenham kutoka sare kwa 2-2 na Chelsea jumatatu na kushindwa kusogea mbele kwa point kwani Leicester inaongoza kwa point 77.

Leicester City ilikutana na Manchester United, Jumapili ya Mei mosi katika uwanja wa Old Trafford na kulazimika kumaliza mpira kwa sare ya magoli 1-1.