Lebo ya Mandevu Records kuwatambulisha Wazenji Classic karibuni

0

Lebo ya muziki wa kizazi kipya visiwani Zanzibar ya Mandevu Records, hivi karibuni imesema italitambulisha kundi jipya kutokea katika studio hizo za Mandevu Records ambao wanakwenda kwa jina la Wazenji Classic.

wazenji classicAkiandika kupitia ukurasa wake wa Facebook mtayarishaji wa studio hiyo Buju mandevu, amesema kuwa baada ya kuwatambulisha baadhi ya wasanii ambao kwa sasa wanafanya vizuri kutokea studio hapo kama Cool Kaka, Alpha Da Best na Man Chado.

“Wazenji Classic ni kundi jipya ambalo litatambulishwa hivi karibuni ambapo watakuja na wimbo wao unaitwa Ndoto” Amesema Buju.

Kwa upande mwingine Mtayarishaji hakutaka kutaja idadi na majina ya wasanii wanaounda kundi hilo na kutaka iwe ‘surprise’ kwa mashabiki.