Laki wa Promise ateuliwa kuwa rais wa chama cha wasanii wa muziki Zanzibar (ZFU)

0

Jumapili ya Septemba 10 viongozi na wanachama wa chama cha wasanii wa muziki wa kipya (ZFU) walifanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wao wapya kwa ngazi ya urais, Makamu wa rais, Katibu mkuu na katibu msaidizi.

ZFU

Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa studio za Rahaleo Zanzibar ambapo wasanii na viongozi wa chama cha wasanii muziki wa kipya kutoka Tanzania bara (TUMA) akiwemo Stara Thomas, Brightone na Witness walikuwa kama wasimamizi wa uchaguzi huo na mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma.

Soma matokeo ya uchaguzi huo hapo chini:

Nafasi ya Urais

Laki wa Promise 34 Mash Marley 9 Iliyoharibika (1)

Nafasi ya Makamo wa Urais

King Abel Ndio (36) Hapana (5) Iliyoharibika (1)

Nafasi ya Katibu Mtendaji

King Pozza Ndio (41) Hapana (1) Iliyoharibika (1)

Nafasi ya Katibu Msaidizi

Buyubaya Mtabiri Ndio (40) Hapana (3) Iliyoharibika (1)