Lady Black na Chibby K wala shavu la kurekodi Stone Town Records

0

Marapa wawili kutokea Zanzibar, Mwanadada Lady Black na Chibby K wapata nafasi ya kurekodi wimbo mmoja kila mtu katika studio ya Stone Town.

lady black

Wasanii hao walipata nafasi hiyo walipokuwa stejini wakifanya ‘freestyle’ kati yao na ndipo uongozi wa Stone Town ulipowaona na kuwaambia kwamba wamewapa nafasi ya kurekodi wimbo bure kwa wasanii.

Mmoja wa msimamizi wa studio hiyo, Badawi alisikika akisema “Nimewaona vijana wengi hapa leo (Disemba 10) wakifanya onyesho lakini nilivutiwa sana na mwanadada Lady Black na Chibby K wana vipaji vizuri na kama nikiwa mmoja wa Stone Town Records tunawapa nafasi ya wao kuja kurekodi wimbo mmoja bure.” Alisema Badawi.