Kwa wapenzi wa tamthiliya ya ‘Empire’, Jussie Smollett (Jamal Lyon) huenda asiwemo tena kwenye tamthiliya hiyo

0

Inawezekana muigizaji wa tamthiliya ya ‘Empire’ Jussie Smollett maarufu kama Jamal Lyon huenda ikawa kwake yeye kuendelea na tamthiliya hiyo kuwa kikomo. Katika igizo hilo linaloonyeshwa kila jumatano na FOX TV huko nchini Marekani ambapo kwa sasa imefikia awamu ya 2 sehemu ya 17 ‘Rise by Sin’ ambapo Jamal akionekana kupigwa risasi bahati mbaya na Freda Gratz. Na muigizaji huyo kuandika katika akaunti yake ya Twitter kuwa hatorudi tena.

https://twitter.com/JussieSmollett/status/730623927395880961

Na aliendelea kuandika katika ukurasa wake

Katika hali ya kushangaza ya taarifa hizo kwenye Twitter yake ziliwafanya mashabiki wake njia panda na kusema kuwa endapo hatoendelea tena kwenye tamthiliya na mashabiki itakuwa mwisho kuangalia kipindi hicho katika FOX TV.