“Kunizalia mtoto ni jambo jema ila tabia na matendo hayanipendezi ” – Kijukuu

0

Msanii wa muziki anaewakilisha lebo ya Waiz Empire, Kijukuu ambae pia ni mzazi mwenzie Angel. Ametoa malalamiko yake kuhusiana tafrani inayowakabili wawili hao juu ya mtoto wao Jonathan baada ya Kijukuu kuonekana kumkataa mtoto.

KijukuuAkizungumza na Zenji255 Kijukuu amesema kuwa, kiupande wake amesema hajamkataa mtoto na yupo tayari kumlea Jonathan ila mzazi mwenza ndie anaemkatalia kumpa mtoto baada ya yeye kukataa kuhusu mtoto na kusambaza maneno machafu juu yake.

“Jambo ambalo amenifanyia mzazi mwenzangu ni kunizalia mwanangu, ila tabia zake siziwezi, nilikuwa natamani kufunga nae ndoa maana ni mwaka mmoja na nusu toka tuwe katika mahusiano. Mimi akinikubalia kunipa mtoto nitamlea tena malezi mazuri tu na yeye mwenyewe pia ataendelea kuwa nae kama mama” Amesema Kijukuu.

Kijukuu kwa upande mwingine pia Kijukuu amepata mtoto wa kike hivi karibuni ambae anaitwa Kauthar ambae amezaa na mkewe.