Kundi jipya la ‘Watafutaji’ kuachia ‘Changamoto’ wiki ijayo

0

Wasanii wa Hip Hop wanaounda kundi la ‘Watafutaji’ Huza B na Buyubaya wanatarajia kuachia wimbo wao mpya kwa mara ya kwanza inayoitwa ‘Changamoto’ Jumatatu ijayo.

watafutaji

Akiongea na Zenji255 Buyubaya amesema kuwa wimbo tayari wameshaurekodi na upo katika maandalizi ya mwisho mwisho na wanatarajia wiki ijayo wataitambulisha kwenye vituo vya redio na sehemu nyingine.

“Wimbo tumefanya katika studio za Mr T. Touch Bongo (Dar es Salaam), na wimbo upo vizuri tu unazungumzia changamoto zilizokuwepo katika sehemu tofauti za burudani kwa mfano matamasha ya Fiesta, tuzo za Kili na mambo mengi yanayofanyika bongo lakini Zanzibar sisi hatupo kwanini na ukiangalia huku pia wasanii tupo.” Aliongea Buyubaya