Kuna jambo gani linaendelea kati ya I.T na Smile?

0

Kwa siku hivi karibuni wasanii wawili I.T na Smile wameonekana wakitambiana kwenye mitandao na ikafikia hatua mpaka mashabiki kujiuliza ni kitu kilichosababisha ugomvi wao.

I.TKuna baadhi ya mashabiki wanaufananisha ugomvi wa wawili ni kama Diamond na Ommy Dimpoz, wengine husema wanatafuta KIKI ya kutengeneza wimbo wa pamoja. Ila mpaka sasa hatujajua nani ni mkweli.

Zenji255 ilipata fursa ya kuongea na I.T ili kuzungumzia kuhusiana na swala hilo, alisema kwa upande wake yeye hana ugomvi na Smile ila anasema kuwa chanzo cha ugomvi huo ni Smile kuwa na wivu na mafanikio yake baada ya kuachia wimbo na video ya ‘Ushanivuruga’.

“Kiukweli Smile bado¬† ni mdogo sana kwangu na najua hiyo ni moja ya kutafuta kiki kwani ninaamini kaamua kuyasema maneno yale ni sababu ya wivu, labda kwa sababu ya mimi ni ‘legendary’, pengine wimbo wake haujakamalika na hauko sawa kwahiyo anataka wimbo wake uendelee kubakia vitu” Amesema “Kwa ushauri wangu wa kumpa ajaribu kutengenezea mashairi mazuri ambayo yatadumu daima ambapo shabiki wake akisikiliza asichoke kusikilizwa” Alimalizia I.T.