Klabu Bingwa Afrika: Zimamoto waondoka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ferroviario De Beira

0
Katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika, leo katika uwanja huo Timu ya Zimamoto imejaribu karata yake kwa ushinda wa bao 2-1 dhiti ya Timu ya Ferriviario De Beira kutoka Msumbiji. Katika mchezo huo Timu ya Beira imeaza kuandika bao lao la kwanza kupitia mshambuliaji wake Manuel Correira katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo katika dakika ya kwanza.
Timu ya Zimanoto imesawazisha bao hilo kupitia kipindi cha kwanza katika dakika ya 33 ya mchezo baada ya kufanya mabadiliko na kuzaa matunda ya mabadiliko hayo na kuandika bao lao la kusawazisha kupitia kwa mchezaji wake Khatib Said, hadi mapumziko timu hizi zimetoka sare ya bao 1-1.
 Kipindi cha Pili kilianza kwa kila upande kushambulia gali la mpizani wake hatimae katika dakika ya 65 ya mchezo huo kipindi cha pili timu ya zimamoto imefanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji wake Hakimu Khamis. hadi mchezo huo unamalizika timu ya Zimamoto imetoka kifua mbele. kwa ushindi wa bao 2-1